MKUDE AWAAMBIA HAYA WANASIMBA
Zainabu Rajabu.
WAKATI joto na presha ikiendelea kukua juu ya mtanange wa Nusu Fainali ya FA kati ya Azam FC na Simba. Nahodha wa Simba, Jonas Mkude ameibuka na kuwaambia mabeki wa timu haya.
Mkude amewaambia mabeki wa timu yake lazima wamuwekee ulinzi imara mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ kwenye mchezo utakaopigwa Kesho.
Simba na Azam FC zitavaana wekeendi hii katika Nusu Fainali Kombe la FA, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba imefuzu hatua hiyo baada ya kuiondosha timu ya Madini ya Arusha kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye Robo Fainali iliyopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Azam FC iliitoa Mtibwa Sugar kwa kuichapa 3-0 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Bingwa wa michuano ya FA anapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza Shaffidauda.co.tz. Mkude alisema mabeki wa Simba wanatakiwa kumtupia macho kila mara mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco kwa kuwa straika huyo hana masihara na lango la wapinzani wake.
Alisema Bocco amekuwa akiwafunga mara kwa mara kutokana na kutoweka ulinzi imara kwenye mechi wanazokutana nazo.
Mkude, alisema Bocco ni mshambuliaji hatari kwenye michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Kombe la FA hivyo hatakiwi kufanyiwa masihara wakati akiwa uwanjani.
Nahodha huyo amesema Simba itakuwa na matumaini ya kushinda mechi hiyo kama mabeki wake watamuwekea ulinzi straika huyo kwa kuwa ana historia nzuri ya kuifunga timu yao.
Aidha, Mkude alisema Simba haitokuwa mteja kwa Azam FC kama ilivyokuwa kwenye mechi iliyopita ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Simba ilichapwa 1-0, bao lilifungwa na John Bocco.
“Tuna matumaini ya kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Azam FC lakini hofu yetu ni kwa Bocco, kama tunahitaji kupata ushindi wa haraka basi lazima tumzuie,” alisema Mkude.
Bocco amekuwa kwenye historia nzuri ya kuifunga Simba kwenye michuano yote wanayokutana nayo ambapo hadi sasa ameshaifunga mara 19.
Straika huyo amerudi uwanjani hivi karibuni baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi Mbambane Swallows hatua ya mtoano
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: