MZEE WA MIAKA 71 AMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI (9)HUKO MBWEWE
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, wa
kwa kushoto akizungumza na baadhi ya waandishi mkoani hapo.
Baadhi
ya waandishi wa habari mkoani Pwani, wakimsikiliza kamanda wa polisi
mkoani humo, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga. (picha na
Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MZEE
Athuman Ramadhan Njuila ,miaka 71 ,mkazi wa Mbwewe,Bagamoyo,mkoani
Pwani anashikiliwa na jeshi la polisi, kwa kosa la kumbaka mtoto wa
miaka Tisa, mwanafunzi wa darasa la pili.
Mzee
huyo alifanikuwa kufanya unyama huo baada ya kumrubuni mtoto huyo
aingie ndani ya nyumba yake kusikiliza muungurumo wa mashine.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alieleza mtuhumiwa alimwambia mtoto huyo aingie ndani kisha alimsukumia kitandani na kuanza kumwingilia kimwili.
Kamanda
Lyanga, alisema taarifa hizo walizipata kutoka kwa wasiri kuwa kuna
mtoto wa shule amebakwa lakini familia zao zimeanza mazungumzo ya
kumalizana kimya kimya juu ya tukio la binti yao.
"Baada
ya kupata taarifa hizo, tarehe 24 april mwaka huu, jeshi hili,
tulimhoji mama mzazi wa binti huyo ambae alikiri kutokea kwa tukio hilo
"alisema.
Kamanda
Lyanga, alitoa wito kwa wananchi kuacha kutoa mazingira rafiki kwa
wabakaji ili kukomesha vitendo vya ubakaji kuanzia ngazi ya familia.
Alisema
endapo vitendo hivyo vikitokea inapaswa kutoa taarifa polisi haraka
iwezekanavyo ili muathirika wa tukio aweze kupatiwa matibabu mapema,
ikiwemo kukusanya ushahidi na mtuhumiwa kuchukuliwa hatua kwa wakati.
Kwa
mujibu wa mtoto, alifafanua kwamba,siku hiyo alifika kwenye nyumba ya
babu na kumkuta akiwa na bibi yake kisha baada ya muda bibi aliondoka na
kumuacha akiwa na babu yake ndipo alipofanyiwa kitendo hicho.
Kufuatia
kutokea kwa tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapo, limefanikiwa
kumkamata mtuhumiwa Njuila, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa na
mtoto huyo alipatiwa PF3 kwa ajili ya matibabu.
Katika
tukio jingine, kamanda Lyanga alieleza, mtu mmoja mwanaume,
(23)ameuawa,kwa kuchomwa moto na watu wasiofahamika kisha mabaki yake
kutupwa katika eneo la vichaka vya shirika la elimu Kibaha.
Alisema
jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa mlinzi wa shirika kuwa ameona
mwili katika vichaka vya shirika ukiwa umechomwa moto.
Jeshi hilo lilikagua eneo la tukio ambapo ilionekana kuwa mtu huyo aliuawa eneo jingine na kwenda kutupwa kwenye eneo hilo.
Marehemu
ametambuliwa na ndugu zake kuwa anaitwa Oscar Charles Swea
(23),msukuma, mkazi wa jiji la Dar es salaam na alikuwa ametoweka kwao
kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: