Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Shinyanga katika wilaya ya Kahama, imeziruhusu halmashauri za Msalala na Ushetu kuanza kuteketeza wanyama wakali aina ya fisi, wanaotishia usalama wa wananchi
Taarifa hiyo ilitolewa kwa vyombo vya habari hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege akisema kuwa wameanzisha operation maalumu ya kutokemeza fisi hao kwa kuwaua kwa kutumia sumua na bunduki.
“Fisi hao wakiingia katika vijiji huwatishia maisha wanawake pamoja na watoto ila kwa upande wa wanaume, fisi wamekuwa wakiwaogopa” alisema Berege
Hadi sasa fisi wapatao 14 wameuwawa, kutoka Kijiji cha Kakola waliuawa fisi saba, Kata ya Ngaya fisi sita na Kata ya Chela aliuawa fisi mmoja
No comments: