JINSI YA KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MPENZI ALIYE MBALI

Image result for MAHUSIANO

Futalia somo hili natumaini litakusaidia kwa neema ya Mungu.
Ni wazi kila mmoja anapenda kufurahia maisha akiwa karibu na mpenzi wake ,hakuna mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake halafu akapenda kuwa naye mbali. Wapendanao hupenda kuwa pamoja wakionana na kujadili mambo mbalimbali huku kila mmoja akitaka kumuonyesha mwenzake ni jinsi gani anavyompenda.
Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo iwapo utazitumia kwa umakini basi jua mahusiano yako yatahimili umbali na upendo wako na mpenzi wako utazidi kuwa madhubuti.

1.MAWASILIANO YA MARA KWA MARA
Mawasiliano ni moja ya nguzo muhimu sana katika mapenzi zinazofanya mapenzi kuweza kustahimili umbali. Wapenzi wanashauriwa kuwa na kawaida ya kuwasiliana mara kwa mara ili penzi liendelee kuwa na ustawi mzuri,kwan unapokuwa na utaratibu wa kuwasiliana na mpenzi wako mara kwa mara unaufanya ubongo wako usimsahau na kumfanya pia kutambua kuwa unampenda hivyo kujiweka mbali na vishawishi au kumpa nguvu ya kukabiliana navyo.

2.USIWE NA MTAZAMO POTOFU
Unapokuwa na fikra kuwa huko mpenzi wako aliko anakusaliti,maana yake utakuwa unapunguza kiwango cha uaminifu kwake,kitu ambacho mara nyingi hupelekea mapenzi kupungua. Watu wangapi wanaishi karibu na wapenzi wao lakini bado wanasalitiwa? Hivyo ukichukulia kigezo cha mpenzi wako kwa kuwa yuko mbali eti anakusaliti utakuwa unakosea sana,mtu anapoendekeza fikra potofu juu ya mpenzi wake husababisha hata matamshi na vitendo vyake dhidi ya mpenzi wake kubadilika na matokeo yake ni kuingia katika migogoro itakayokuwa na nafasi kubwa ya kuharibu penzi lenu.

3.TAFUTA VITU VYA KUKUWEKA BUSY
Ikiwa labda umezoea kutoka na mpenzi kwa ajili ya matembezi au chakula cha jioni na kipindi hicho hayupo,unachotakiwa kwa muda huo ni kuomba kuchati nae ili akuondolee upweke au kama hiyo haiwezekani kutokana na asili ya kazi yake au eneo alipo basi unaweza kuamua kutumia muda huo kwa kuangalia filamu au kucheza game kwa ajili ya kujiepusha na upweke.

4.JIAMINI
Kitu kingine ambacho huwa kinasababisha watu kuona kuwa wapenzi wao kuwa mbali nao ni sawa na kuwasaliti,ni vitendo vyo vya kutojiamini,utakuta mtu haamini kabisa kama uhusiano wake kama uko salama eti kisa mpenzi wake yuko mbali. Hivi jamani naomba kuwauliza wana APPLE hivi mpenzi wako alivyokubali kuwa na wewe ulimshikia bunduki au panga ili akubali? Bila shaka jibu ni hapana sasa kama ndivyo kwanini unataka kufa kwa shinikizo la damu eti kisa mpenzi wako hayuko karibu na wewe? Jamani utakaposhindwa kuijiamini katika mahusiano yako ,basi umbali utakuwa ndo chanzo kikuu cha kukuachanisha na mpenzi wako.

5.TUMIENI MUDA MWINGI KUWA PAMOJA KILA MNAPOPATA NAFASI
Ili kuweza kutengeneza misingi imara ya mapenzi yenu,unapopata fursa ya kuwa na mwenzi wako iwe kwa ajili ya likizo au kitu kingine inabidi mtumie muda mwingi kuwa pamoja. Kitendo cha kutumia muda mwingi pamoja maana kitendo hiki kitawasaidia kuwaondolea wasiwasi juu ya kusalitiana kipindi mlichokuwa mbalimbali. Pia katika kuwa kwenu pamoja inatakiwa ujiepushe na lawama au aina yeyote ya shutuma dhidi ya mwenzako badala yake unapaswa kuongelea ni kwa kiwango gani ulivyommisi na unavyoumizwa na kitendo cha kuwa mbalimbali.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.