RAISI WA AFRIKA KUSINI AKATAA KUONDOKA MADARAKANI

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekataa mwito wa kumtaka aondoke madarakani, akisema hatma yake inatakiwa kuamuliwa na wananchi.
Rais Zuma amesema ataondoka madarakani kama raia walio wengi wa Afrika Kusini wakimtaka aondoke. Ameongeza kwamba baadhi ya watu wanamtaka aondoke madarakani kutokana na yeye kusema ukweli.

Kauli hiyo imekuja kufuatia maandamano ya kumpinga yaliyoanza tarehe 7 mwezi huu baada ya rais Zuma kuwafuta kazi waziri wa fedha Bw Pravin Gordhan na mawaziri wengine tisa Machi 31.

Kutokana na hatua hiyo mashirika ya kimataifa ya kutathmini uwezo wa kulipa madeni Standard & Poor’s na Fitch yameshusha viwango vya Afrika Kusini.

Zuma amesema ataendeleza mageuzi ya kiuchumi ili kutatua matatizo yaliyopo kwa muda mrefu.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.