VIDEO: HAYA NDIO MAAMUZI YA MAHAKAMA YA ARUSHA KWA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UVCCM ARUSHA

Image result for Mahakama ya Arusha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo April 28, 2017 imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kutumia kitambulisho cha Usalama wa Taifa.

Hakimu Gwanta Mwankuga ambaye alikuwa anasikiliza kesi hiyo, amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kupeleka mashahidi katika kesi hiyo na kusema Mahakama haijamuachia huru mshtakiwa kwa ombi la Jamhuri kutaka kuondoa shitaka hilo Mahakamani, bali amemuachia kwa kifungu cha sheria namba 225 kipengele cha 5.

Ayo TV na millardayo.com imempata Charles Abraham ambaye ni Wakili wa Lengai Ole Sabaya na hapa anafafanua zaidi kuhusu kesi hiyo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.