WATU 21 WAFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NCHINI IRAN

Waokoaji nchini Iran
wameopoa miili ya watu 21 baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika mgodi mmoja wa makaa ya mawe, huku zaidi ya wengine 69 wakijeruhiwa.

Mlipuko huo unadhaniwa kusababishwa na kuvuja kwa gesi katika mgodi wa Zemestan-Yurt Kaskazini mwa jimbo la Golestan.

Baadhi ya miili hiyo ni ya watu waliokwenda katika mgodi huo kuwasaidia waliojeruhiwa.
Zaidi ya wachimbaji wengine 32 wamekwama ardhini.

Juhudi za uokoaji zinaendelea huku zikikwamishwa na njia nyembamba ya kuingia sambamba na uwepo wa kiwango kikubwa cha gesi ndani ya mgodi huo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.