BABU AMBAKA MJUKUU WAKE NA KUMPA MIMBA


Mwanza. Polisi mkoani Mwanza inamshikilia mkazi wa mtaa wa Nyasaka wilayani Ilemela mwenye miaka 66 kwa kumbaka na kumpata ujauzito mjukuu wake mwenye umri wa miaka 16. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo liligundulika Aprili 25. 

Alisema mwanamume huyo alikuwa akiishi na mjukuu wake (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Nyasaka. 

“Mtuhumiwa alikuwa akiishi na mjukuu wake tangu mwaka 2011 akitokea Musoma vijijini na alikuwa akimfanyia ukatili wa kingono kwa kumwingilia kimwili wakati mkewe hayupo,” alisema Msangi. 

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa alikuwa akimtisha kuwa atamwachisha shule na kumrudisha kijijini kwao mjukuu wake endapo atatoa siri kwa mkewe au ndugu zake. 

Msangi alisema kutokana na vitisho hivyo, binti huyo aliendelea kuvumilia hali hiyo pasipo kumwambia mtu na Aprili 25 walimu walitilia shaka hali ya afya yake na alipopelekwa hospitali kupima iligundulika ana ujauzito wa miezi minne. 

“Walimu walimhoji aliyempa ujauzito na alidai ni babu yake. Walitoa taarifa kituo cha polisi ambapo walifanya ufuatiliaji na kumkamata mtuhumiwa,” alisema Msangi.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.