RAISI MAGUFULI KUPOKEA TAARIFA YA VYETI FEKI LEO




Rais Dkt. John Pombe Magufuli siku ya leo Ijumaa anatarajia kupokea ripoti ya taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa Umma ambayo itawasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema anasubiri ripoti ya Watumishi wa serikali ambao wanavyeti feki ili awashughulikie huku akidai kuna watu zaidi wa elfu tisa wana vyeti feki. 
Rais Magufuli atakabidhiwa ripoti hiyo leo kwenye ukumbi wa Chimwaga, Dodoma 

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.