JE, SIMBA SC ITATINGA FAINALI LEO?


KOCHA MSAIDIZI WA SIMBA, JACKSON MAYANJA.

TIMU mojawapo itakayokaribia kufuzu kushiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani inatarajiwa kujulikana katika mechi ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA kati ya Simba dhidi ya Azam FC itakayofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshindi katika mechi hiyo atakutana katika fainali ya mashindano hayo itakayofanyika Mei 27 mwaka huu dhidi ya mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili itakayowakutanisha mabingwa watetezi Yanga dhidi ya Mbao FC kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema jana kuwa kikosi chake kimejiandaa vyema kuikabili Azam FC ambayo hivi sasa imewekeza nguvu zote kwenye michuano hiyo.

Mayanja aliongeza kuwa Simba watapambana ili kushinda mchezo wa leo na kuendelea kuwa kwenye nafasi ya kushinda kombe hilo pamoja na ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao unashikiliwa na Yanga pia.

"Sisi tuna nafasi mbili lakini wenzetu Azam wamebakiza hii moja, tunajua mpira utakuwa mgumu lakini tunaamini huu ni wakati wetu wa kuibuka na ushindi," alisema Mayanja ambaye jana asubuhi pamoja na Kocha Mkuu Joseph Omog walisimamia mazoezi kwenye Uwanja wa Bigwa na jioni walirejea Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa Azam, Iddi Cheche, alisema mechi ya leo kwao ni zaidi ya fainali kwa sababu wanataka kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani na vile vile kuendelea kushinda mataji msimu huu.

Cheche alisema kuwa kila mchezaji wa timu hiyo anafahamu umuhimu wa kushinda mchezo huo ili waendelee kushiriki michuano ya kimataifa na vile vile kutangaza vipaji vyao nje ya Tanzania.

Hata hivyo, Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwamkemwa, alisema kuwa nafasi ya nahodha na mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo John Bocco kucheza katika mechi ya leo iko 50-50.

Refa wa kati katika mechi hii ni Mathew Akrama kutoka Mwanza atakayesaidiwa na Omari Kambangwa na Michael Mkongwa.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.