SHERIA 10 ZA KUMRIDHISHA MWANAUME WAKO KIMAPENZI

Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo barabara!


Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani. Sasa swali linakuja…..Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo, Bi. Layla amekuja na sheria 10 zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.
1 Vaa vizuri. 
Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.
2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana.
 Mwaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.
3 Fanya mazoezi na onekana Bomba.
Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la kumpelekesha kirahisi kitandani, Basi!

#4 Kuwa Mchokozi.
Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake.

#5 Jiamini na Jipende.
 Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.


#6 Kuwa mdadisi wa tendo zima la kujamiiana na kuwa mbunifu.
Kufanya mapenzi ni raha, na ni tendo nyeti kati ya wapenzi wawili. Hivyo basi, jaribu mambo mapya kadri unavyoweza na usije ukabaki na nyenendo zile zile kila siku (stuck in a routine), hata kama unajisikia vizuri na mapozi au nyenendo hizo (even if it feels comfortable).

#7 Mtomase kwa namna anavyopenda yeye.
Wanaume wengi hawapendi kutomasana (foreplay). Tunalijua hilo kwa muda mrefu, lakini huenda ni kwasababu tunaomba kutomaswa sehemu ambazo si sahihi kwa mtazamo wake. Kwa wanawake, kutomasa kuna maanisha kupapasa na kunyonya sehemu mbalimbali za mwili. Lakini, pengine kuna vitu vyengine au kutomasana kwa aina nyingine, ambayo mwanaume wako anaweza kupenda (enjoy). Mathalani, unaweza ukamruhusu mwanaume wako akupige masaji kwa mafuta ya kunukia au kukuchora kwa hina, au pengine unaweza ukamruhusu akupige picha za utupu wakati mnatomasana (lazima umuamini vya kutosha kabla ya kumruhusu kupiga picha za utupu, kwani kama dume ni bwege basi picha utazikuta kwenye magazeti ya udaku kesho yake!). Pointi hapa ni kwamba kuna namna nyingi sana za kutomasana, kwahiyo tafuta ni namna gani mwanaume wako anapenda, na tumia hiyo kumridhisha! Vinginevyo, vicheche watamchukua.
8 Ongea kimahaba (Talk dirty).
Wanaume wanapenda mwanamke, ambae anaongea uchafu kitandani kiasi kwamba jogoo anawika kwa kumsikiliza tu asemayo. Kama unataka kujua namna ya kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi unatakiwa kujua kuongea uchafu. 

9 Usisome gazeti wakati wa kufanya mapenzi. 
Toa milio ya kimahaba wakati unafanya mapenzi na mwanaume wako, kwa maana nyingine usikae kimya kama unasoma stori Fulani ya kusisimua kwenye gazeti. Toa miguno wakati anakubusu busu shingoni, na toa miguno wakati anakwenda deeper! Hii inamsisimua sana mwanaume, na anatendelea kujituma kwa bidii zote.
10 Wasiliana (Communicate!).
Mawasiliano ni muhimu sana linapokuja suala la mapenzi, hakuna ubishi katika hilo. Muulize mwanaume wako anapendelea mikao gani, sio tu kwamba atakupa jibu, bali itamhamasisha nay eye kukuuliza unapendelea nini. Mkijijengea misingi ya kuulizana, basi hamtokuwa na ulazima wa kuhisi au kubuni kinachohitajika. Source: LovePanky

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.